Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mkusanyiko wa Wanazuoni wa Jabal Amil nchini Lebanon katika ujumbe wake kwa mnasaba wa “Eidul Ghadir” umesisitiza kwamba Lebanon, chini ya mwendelezo wa mashambulizi na vitisho vya Israel, pamoja na udhaifu wa mamlaka rasmi na ukimya wa kutia shaka wa kimataifa, Kiarabu na Kiislamu, inakabiliwa na kipindi hatari.
Mkusanyiko huo umesisitiza kwamba; wananchi wa Lebanon, licha ya kuhamishwa kwa kulazimishwa, mateso na mashinikizo ya kiuchumi, kwa mara nyingine wameonesha mshikamano wao na uchaguzi wa kusimama imara, mshikamano na Muqawama; huku jeshi la Lebanon likizuiwa kutekeleza kikamilifu jukumu lake kutokana na mashinikizo na maelekezo ya nje.
Katika taarifa hiyo pia kumetolewa wito wa kuimarishwa umoja wa kitaifa na kushikamana na nguzo za nguvu za ndani, ambapo mbele yake ni wananchi na Muqawama kwa yale yanayoonyesha uwezo wa kuzuia na kusimama imara, pamoja na jeshi kama taasisi ya kitaifa inayowajumuisha wote. Aidha, taarifa hiyo imekataa miradi ya kuchochea fitna, kuhalalisha uhusiano na kujisalimisha, na ikasisitiza kwamba; maadili ya Ghadir yataendelea kuwa nembo ya haki, heshima na kupinga ubeberu pamoja na uvamizi wa kigeni.
Maoni yako